December 8, 2017


Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani sasa atakaa nje kwa wiki mbili.

Yondani ni majeruhi, ameumia wakati akiitumikia timu ya Tanzania Bara inayoshiriki michuano ya Chalenji.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema jopo la uuguzi la Kilimanjaro Stars limewataarifu kuhusiana na kuumia kwa Yondani.

“Daktari wa Kilimanjaro Stars amesema Yondani ameumia na atakaa nje kwa wiki mbili. Hivyo tunaendelea kusubiri ripoti maalum,” alisema.


Yondani ni tegemeo la ulinzi katika kikosi cha Yanga, Kilimanjaro Stars na Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic