December 14, 2017




Charles Marwa (42) mwenyeji wa Bujingwa, Mwanza ndiye mshindi wa droo ya 37 ambaye juzi alikabidhiwa TVS King Deluxe mpya kabisa kutoka SportPesa ambayo alijishindia kupitia droo ya promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA. 

"Mimi nimekuwa mpenzi wa kubeti na sportpesa tangu imeingia Tanzania, ila sasa mke wangu  alikuwa anabisha sana ila nikamuhamasisha akaanza kucheza. Na Mungu saidia akaweka mkeka wa timu 11 Multi Bet, alivyoweka hiyo kwakweli  alipiga milioni saba. 

"Lakini nashukuru Mungu tena, baada ya mwezi mmoja tena, katika ile "betting" yangu, nimebeti nimekosa lakini siku moja  nikapigiwa simu.   Sikuamini, kwa kweli mpaka imefika hapa  (TVS King) ndiyo nimeamini.

"Uzuri wa SportPesa, MultiBet wanakuwekea soko moja, hao wengine wanatenganisha masoko. Unaweza kuchagua timu hii itashinda au timu nyingine itashinda, lakini yote yatakuwa kwenye soko moja. 

"Kwakweli hii bajaji sijalipia hata senti tano, hapa nilichoombwa ni TIN namba na namba za kitambulisho. Bajaji hii nimeletewa mpaka hapa niliposimama, imetoka Dar es Salaam mpaka hapa Mwanza, sijalipia hata shilingi moja. 

Kwa shilingi elfu mbili ambayo nilibetia, imenifikia hapa. Mimi huwa natumia njia ya mtandao kila mara tangu nimeanza kubeti." alisema mshindi huyo ambaye kwa sasa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo.

katika kutia mkazo juu ya uhalali wa michezo ya SportPesa, mke wa mshindi bi. Happiness Charles Marwa alifunguka na kusema,

"Nimewahi kushinda lakini (Charles) huwaga ananisaidia kucheza. Mimi sio mzoefu sana wa hii michezo isipokuwa yeye ndiye ananisapoti kutabiri zile timu. Siku hiyo alinisapoti akanielekeza ndiyo nikawa nimepata hiyo milioni saba ambayo nilifungua duka na nilinunua shamba."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic