Mwanachama wa siku nyingi wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali ameshangazwa na wale wanaotaka avuliwe uanachama na kusema hawana jeuri hiyo.
Pamoja na kuibuka na kusema hivyo, Akilimali amesema kama atafanyiwa figisu na kuondolewa Yanga, yeye na wazee wenzake watakwenda hadi ikulu ya Rais Magufuli na kufikisha malalamiko yao.
Leo mchana, baadhi ya wanachama wa Yanga walitaka Akilimali kuondolewa uanachama kwa kuwa amekuwa akizuia mabadiliko ya klabu hiyo.
"Nimezuia mabadiliko yapi, mimi ni kati ya wale tuliotaka mabadiliko hata wengine hawajawa wanachama.
"Tatizo hawa wenzetu wanataka mambo ya haraka na ili mradi kuwaridhisha watu. Lazima tufuate utaratibu na hii ni lazima.
"Kama wanataka kuigawa klabu wanajidanganya na mimi na wazee wenzangu kamwe hatuwezi kukubali," alisema.
MZEE...AKILI...MALI!!!!
ReplyDeleteHuwezi sema hajui analolifanya ila labda iwe makusudi. Kama anachosema ni kweli kwamba watu wafuate utaratibu mi namuunga mkono...ila kama ana jambo lingine nitakuwa kati ya wale wanaompinga.
Kwanini????
Mara ya kwanza naanza kuifatilia Yanga tangu nacheza cha ndimu miaka ya themanini sikuwahi kumsikia katika mfumo wa mpira. Huwa mabadiliko yanawaibua wengi sana. Kipindi cha Mpondela hadi Nchunga sikuwahi kumsikia..ila nimeanza sana kumsikia wakati yupo Manji.
Mzee Akilimali anaweza kuwa na busara zake katika uendeshaji wa "Club" ili isiwe busara inayoweza kuwakera wengine. Usiwe mwanafunzi ambaye kila mwalimu anachoongea na kuuliza unataka kujibu wewe tu darasani...wengine watakuchoka.
Ningekuwa mimi ndio huyu mzee..ningekaa kimya ili nione ni nini wanachotaka kukifanya. Maendeleo ni jambo la msingi mzee. Usije ukawa kama wale wazee wengine ambao wao kwa kuwa walienda shule bila kula wanataka hata watoto wao waishi hivyo...hii ni miaka mingine.
Tunahitaji mpira uje katika mabadiliko..tunataka timu ziendeshe kisayansi na si kama tulivyozoea. Hatufiki mbali kwasababu ya haya mambo. Acha watu wasongeshe kurudumu. Mi nasema kama kuna mtu anakupa nguvu sasa nae achoke maana kila mtu anakulalamikia wewe tu jamani.
Na kama kuna mtu ambae anatumika kurudisha ili suala nyuma akemewe..na aiache timu. Mi naamini utakuta hata si mwanachama wa Yanga. Akiona timu inateseka kwake ndio furaha yake. Hili lingekuwa limeisha kama Manji angekuwa ameachiwa timu. Si kila mfumo wa uendeshaji tuseme wenzetu hawafanyi hivyo. Mwenzako we nani??unataka kujifananisha na Muingereza???sisi tuendeshe kwa mfumo tunaoutaka. Kama timu kukodisha ikodishe...kikubwa mpira ucheze na wachezaji wapate chao.
Ooooohhh!!!huu mfumo mpya...we unafananisha na mfumo upi wa uendeshaji. Utanitolea mfano Manchester United...wewe upo Manchester hapa?? mi naendesha timu yangu kwa maslahi ya wakati huo. Mfumo wa Ulaya waachie wenyewe wa Ulaya
Good point, in short huyu mzee anakera mpka nikimuona napata kinyaa, kweli yanga yunayoipenda yakusumbuliwa na taka taka ngoma na isiwe na nguvu ya kuvunja mkataba!kweli ya kumsajiri nkomola kwa mbwembwe, we can't be serious wajamen. Kweli tukapambane na mazembe kwa kumtegemea chirwa tu na ajibu? Bora hats tusishiriki
Delete