December 31, 2017


Pamoja na kutoa pole ya kuumia kwa mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku, kiungo wa zamani wa timu hiyo Paul Scholes ameionya timu yake hiyo na kocha wake, Jose Mourinho.

Scholes ambaye sasa ni mchambuzi katika runinga, ameionyesha Man United kwamba isipojipanga, itakosa hata Top Four ambazo ni nafasi za nne za juu katika msimamo wa ligi.

Scholes amesema mwenendo wa Man United sare na vipigo, unaonyesha kuwa hautakuwa mzuri kama utaendelea.

Amemuonya Mourinho kwamba mwendo huo utakuwa ukiwavunja morali wachezaji hasa baada ya mashabiki kuanza kuwazomea.

Mashabiki wa Man United walizomea wakati timu yao ilipolazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa Old Trafford.


Lukaku naye aliumia wakati akiwania mpira na kutolewa nje kwa machela na akiwa amefungwa kifaa maalum kumsaidia kupumua baada ya kuzimia. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic