December 8, 2017



Pamoja na kocha wake kutamka wazi kuwa hana mpango wa kuendelea kumtumia ndani ya kikosi cha Lipuli FC kutokana na utovu wa nidhamu, kiungo wa timu hiyo, Salum Machaku amefunguka kuwa hana taarifa yoyote kama anatakiwa kuondoka ndani ya kikosi hicho na ataripoti kambini kama wachezaji wengine.

Kiungo huyo kabla ya ligi kusimama alisimamishwa kwa muda ndani ya timu hiyo kutokana na madai ya kukutwa akiwa amelewa baada ya mchezo na kusababisha kukosa mchezo dhidi ya Simba.

Machaku amezungumza na gazeti hili na kusema ataendelea kubaki katika timu hiyo na hana taarifa yoyote ya kuachwa ndani ya timu hiyo

“Ninachokifahamu kwa sasa natakiwa nirudi kambini  kesho Alhamisi (jana) kwenda kuendelea na mazoezi  ambayo wameanza Jumatatu na najua kuna wengine bado hawajafika kama mimi,” alisema Machaku.

Upande wa kocha wa timu hiyo, Selemani Matola  alisema: “Nimefunga mjadala kuhusu Machaku sihitaji mchezaji ambaye anataka kuirudisha timu nyuma na ripoti ya kutomuhitaji nimewasilisha kwa uongozi.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic