December 28, 2017



Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djuma ameweka msimamo wake kuwa kikosi chake kitacheza kwa ushirikiano na hakutakuwa na staa mkubwa kuliko timu.

Djuma ambaye anashikilia nafasi ya kocha mkuu baada ya kufutwa kazi kwa Joseph Omog, amesema anapambana kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wake lakini hatataka kuona kuna makundi.

“Kuwa na wachezaji ambao ni muhimu zaidi ya wenzao, hili si jambo jema. Hakutakuwa na mambo hayo na zaidi ningependa ushirikiano na upendo.

“Hii timu ni yetu sote, lazima kuwe na ushirikiano kuhakikisha tunafikia lengo na ndilo lengo la kila mmoja wetu,” alisema.


Kocha huyo raia wa Burundi, ametokea Rayon Sports ya Rwanda ambayo alifanikiwa kuopa makombe mawili ya ubingwa wa ligi na Kombe la Amani kama Kombe la Shirikisho hapa nyumbani.

1 COMMENTS:

  1. UKIONA MWENZIO ANANYOLEWA.....:::
    Hii ndio sentensi ambayo itakuwa nyuma ya Djuma...sitaki kusema nae atashindwa..ila namwambia Watanzania hatuna uvumilivu. Kama amefukuzwa kocha ambae hajafungwa hawawezi kukuvumilia wewe utaefungwa sasa. Sijui kama unawajua vizuri Watanzania????sijui kama umewasoma hata kwenye vitabu???sisi tumechelewa kupata maendeleo. Tunahitaji maendeleo kwa haraka. Tumekuwa tunaweka ndoto zetu za usiku katika uhalisia. Tunahitaji tuone Tanzania inakuwa Marekani au Dubai kwa ghafla..tunahitaji tuone ndoto zetu zikitimia kwa ghafla...kwa ujumla tunalazimisha.

    Simba iliyokuwa na uwezo wa kujenga kikosi chake kuanzia ngazi ya chini leo tunahitaji kufanya mambo kwa haraka hii ni hatari...Simba tuliyohisi inataka kufanya mambo yake kwa uweredi leo imebadirika. Manara anakuchekea ila siku ya kuondoka atakusaidia kukubebea begi na kukupeleka Mwalimu Nyerere International Airport. Timu zetu kubwa zina watu...zina wachezaji wakubwa kuliko Simba..kama unabisha baada ya miezi miwili we mwenyewe utaanza kuwabembeleza wachezaji. Utakapoambiwa Okwi anahitaji kucheza alafu we unahisi Mo Ibrahim ni bora zaidi. Utakapoambiwa Asante Kwasi anahitajika kucheza wakati we umemuona Mlipili ni bora zaidi. Hapo ndipo tutakapoona habari mpya magazetini. Na waandishi kazi yao ni moja tu...kuwasilisha mada juu ya magazeti...kwa kuweka kichwa cha Habari Kikubwa..."YALIYOMSHINDA FISI"...alafu kazi yetu sisi ni kusoma na kuendelea na stori zetu za vijiweni..."ALIKUJA KWA MBWEMBWE NA KUONA MWENZIE HAJUI"...

    KAZI NI KWAKO (POWER TO YOU)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic