December 28, 2017


AC Milan inayonolewa na Kocha Gennaro Gattuso imeanza kuamka na kujifariji baada ya kuitwanga Inter Milan kwa bao 1-0 katika mechi ya Kombe la Italia.

Bao hilo la Patrick Cutrone lilipatikana katika dakika za nyongeza huku ikionekana kama mechi hiyo ilikuwa inamalizika kwa safe ya 0-0.

Gattuso mwenye furaha kubwa alisema mechi hiyo ilikuwa muhimu kwao pia kuinua hali ya kujiamini na kuendelea kufanya vizuri zaidi mbele.

Inter Milan na AC Milan zina ushindani mkubwa kutokana upinzani wao kihistoria katika soka la Italia.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic