December 28, 2017




Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, umesema mshambuliaji wake, Obrey Chirwa atareja nchini siku yoyote baada ya kwisha kwa msiba wa mtoto wa Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina.

Chirwa aliondoka nchini baada ya kuomba ruhusa kurejea kwao Zambia kwa masuala ya kifamilia. Lakini baadaye akagoma kurejea nchini akitaka kumaliziwa fedha zake za usajili.

Hali hiyo ilisababisha hali ya sintofahamu na Chirwa akaendelea kubaki Zambia huku akionekana mitandaoni akiendelea na kilimo cha mahindi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Salum Nyika amesema kilichomkwamisha Chirwa ni msiba wa mtoto wa kocha.

"Alikuwa bado Zambia, baada ya kusikia kocha ana msimba, alilazimika kubaki kule kumliwaza," alisema akionekana kutaka kupoza kidogo joto la Chirwa kubaki Zambia kwa mgomo.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba, uongozi wa Yanga umemalizana naye kwa kumpatia kiasi cha fedha zake za usajili na umekubaliana naye kurejea haraka.

1 COMMENTS:

  1. MAMBO YA MFICHA UCHI.....:::
    wengine wanasema mficha malazi...sijui nn???haya yote ni mambo ya waswahili. Sisi ni waswahili...waswahili tunaotokea uswahili namambo yetu ni ya kiswahili swahili. Hakuna mswahili unaeweza kumuamini. Wengi tunafanya mambo yetu kiswahili. Ukiambiwa wewe ni mswahili ni neno gumu kidogo maana yake lina ukakasi ndani yake. Mswahili.....kama neno lenyewe..wenyewe wanasema eti..."ni mtu kutoka Pwani ya Afrika Mashariki ambae anatumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano"""..

    Yanga na Chirwa....Chirwa na Yanga...siwezi kusema kuna ukweli au la. Ila kama kuna ukweli basi tuyamalize. Ila kuna hawa wengine ambao majeraha hayakosi. Waombe tu Yanga asiingie bosi kama kule Simba...wataachwa....tatizo lilipo Yanga ni upungufu wa fedha. Si kwamba hawana hela ila wana upungufu wa fedha. Fedha wanazo ila hazitoshelezi. Sasa najiuliza mbona Mbao FC wao wachezaji hawalalamiki au ndio timu ndogo kwenye vyombo vya habari hawauzi. Kwanini Yanga....???kweli kabisa mnasajili kwa mkopo??/Sijajua kama hata Ulaya hii kitu ipo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic