December 17, 2017



Mshambuliaji mpya wa Simba, Dayo Domingues amezua mjadala mkubwa mtandaoni baada ya video yake kusambazwa.

Video ya Dayo imesambazwa mitandaoni na kuonyesha akicheza mechi mbalimbali akiwa na timu yake ya Ferreviario ya Msumbuji.

Baada ya video hiyo, mjadala mkubwa umezuka mitandaoni kwamba kama kweli ni mshambuliaji mkali kama ambavyo imekuwa ikielezwa.

Mbali na hivyo, wako wamekuwa wakihoji kama ni mshambuliaji au wingi kwa kuwa katika video hiyo anaonekana anatokea pembeni kulia.

Lakini wako ambao wamekuwa wakimsifia kutokana na kuonekana ni mwenye kasi.

Simba imemsajili Domingues katika dirisha dogo la usajili ili kuongeza nguvu.

.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic