December 7, 2017




Timu ya Netiboli ya Bunge ya Tanzania, jana asubuhi iliibuka na ushindi wa mabao 13-11 wakiwafunga wapinzani wao Uganda.

Bunge la Tanzania ilipata ushindi huo katika michuano ya Wabunge wa Afrika Mashariki inayoendelea hapa nchini.



Katika mechi hiyo, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Ndani, kila timu ilionyesha ushindani mkubwa kutokana na kuhitaji ushindi.

Mechi hiyo, iliingia doa kidogo baada ya wachezaji wa Bunge wa Uganda kumvamia mwamuzi kwa kile walichodai kuonewa na maamuzi yaliyokuwa yakitolewa.



Wakati wachezaji wakimvamia mwamuzi huyo, Jeshi la Polisi liliingilia kati kwa ajili ya kumuokoa na kuwekwa chini ya uangalizi mkubwa.

Mechi hiyo, ilisimama kwa dakika 20 huku malumbano makubwa yakitawala uwanjani hapo kabla ya mwamuzi huyo kumaliza mechi hiyo kwa Tanzania kushinda mabao 13-11.

 
  

  




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic