December 7, 2017




Kiungo mkabaji wa zamani wa Simba na Timu ya taifa, Taifa Stars, Abdullhaim Humud na Adam Kingwande wametua KMC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Humud anajiunga na KMC katika usajili usajili huu wa dirisha dogo akitokea Majimaji inayoshiriki Ligi Kuu Bara baada ya kuusitisha mkataba wake.

kiungo huyo alionekana akifanya mazoezi ya timu hiyo jana asubuhi kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama Mabatini jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi hayo, alionekana kiungo mwingine aliyewahi kuichezea Simba na Stand United zote zinashiriki ligi kuu akifanya mazoezi ya pamoja na timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Fredy Minziro.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Humud alisema kuwa anafanya mazoezi na timu hiyo baada ya kuwepo kwenye mazungumzo na timu hiyo inayotaka kumsajili katika usajili huu.

“Nipo huku na tarajia kuniona nikiwa naichezea KMC hivi karibuni baada ya kufikia makubaliano mazuri na timu yangu hii mpya.

“Kama unavyoniona nimeanza mazoezi juzi Jumanne baada ya kufikia makubaliano mazuri, kwani KMC ni kati ya timu bora yenye wachezaji wengi wazuri na uzoefu,”alisema Humud.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic