December 18, 2017


Ukisema kimenuka wala hautakuwa imekosea baada ya baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga kutaka kuona mwanachama maarufu wa klabu hiyo anatimuliwa.

Wanachama hao wameonyesha kuchoshwa na tabia ya Katibu wa Baraza la  Wazee wa Yanga Ibrahim Akilimali za kupinga mabadiliko ya klabu hiyo hivyo imewalazimu kutoa mapendekezo ya kumfuta uanachama.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa alitangaza rasmi nia ya klabu hiyo kuanza mchakato wa kwenda katika mfumo wa hisa jambo ambalo baadae Akilimali alisikika akipinga mfumo huo na kuomba Yanga wamtake radhi.

Akilimali amekuwa akishikilia msimamo wake kutaka Yanga ibaki kama zamani na wao wanaona kama anawachelewesha.

Hivyo kutaka Akilimali atupiwe virago na kuiachia Yanga endelee na “maisha” yake.


Akizungumza ndani ya Makao Makuu ya Yanga Makamu  Mwenyekiti wa tawi la Uhuru  Kaisi Edwin alisema,wamekutana wenyeviti wote wa matawi na kukubaliana kuandika barua kwa uongozi huo ili wamfutie uanachama mzee Akilimali

2 COMMENTS:

  1. HAKUNA HAJA:::
    Twende tushindane kwa hoja kikubwa asikimbilie Mahakani. Aende popote..sidhani kama aliposema atakwenda huyo mtu atakuwa anamsikiliza yeye alafu watu zaidi ya milioni wakimpinga. Itakuwa ajabu sana hata mahakama itakayotaka kulizungumza ili suala. Hataki mabadiliko aende. Mbona timu zipo nyingi sana. Yeye anaonma raha timu inavyopata shida???anajickiaje tunavyokuwa ombaomba???mbona asemi iache hivyo alafu atakuwa analipa mishahara yeye???ameshawahi kuja hata na katoni mbili za maji hapo klabuni???

    Tuache figisu..nasema kama kuna mtu anamtumia aache mara moja. Na hili ndio litakuwa jambo la kwanza kulifanyia kazi. Kutafuta wapi huyu mzee anapata nguvu. Hao wazee wengine kama watamuunga mkono nami nitawashangaa sana. Waje..waseme wanaweza kuiongoza timu wenyewe alafu wapewe japo kwa mwezi mmoja tu waone shughuli yake. Mnataka mzee Mkwasa afilisike?? au mnataka Sanga auze mali zake kwa ajili ya timu..? mnaona raha wachezaji wanavyodai mishara? au mnasikia poa Beno anavyosema anataka hela yake ya Usajili???au mnataka mwakani wachezaji wote watukimbie???au mnaona raha Yanga kuwa na kakikosi kadogo vile???

    Yanga si ya aina hiyo bhana.....tunataka mfumo wa maendeleo.Yanga si ya kulia njaa. Aende akasome faida ya business partnership aone. Au kuna ten percent ilikuwa inapatikana pale???tangu Manji aje hali imekuwa mbaya sana kwa wale wapigaji pale. Unakumbuka hawa ndio walisababisha yule Mtendaji wa Kenya aliyetaka kuajiliwa pale akose kazi..anaewekeza anataka watu waaminifu. Mnataka tufanye mambo kwa mazoea. Akaletwa mtu mkajua hapa hatupati kitu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo mzee akapimwe mkojo. Badala awaze kuisaidia yanga yeye anawaza kunufaika yanga,yanga kweli ya kulia lia njaa? Kama anazingua tutamtimua hata kwa fimbo. Sauti ya wengi ni sauti ya mungu. Asitake watu wakufulu kwa ujinga wa mjinga asiye na mbele wala nyuma

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic