Maganga Mosses Mayengo (39) Mkufunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga, aliibuka mshindi wa TVS King Deluxe mpya kutoka SportPesa kupitia droo ya 38 ya Shinda na SportPesa.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Wakufunzi na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga ambapo ndugu Maganga alitoa historia yake fupi ya kucheza na SportPesa mpaka kufikia kuibuka mshindi siku ya Jumamosi tarehe 2 Disemba.
"Nilianza kucheza na SportPesa baada ya kuwa nimesikia kwenye matangazo yao mbali mbali wakijaribu kuelezea kwamba ni mchezo ambao unaweza ukabashiri na kushinda zawadi mbali mbali. Nikaona basi itakuwa ni fursa ya kuweza kushiriki mchezo huu.
"Mwisho wa siku nikiwa nimetulia, sina habari nikapigiwa simu kwamba unaongea na ndugu fulani kutoka SportPesa, nikawa nimepata hisia kwamba inawezekana leo ni siku yangu ya kushinda ile bajaji ambayo kweli nilikuwa nina hamu nayo.
"Nakumbuka siku niliposhinda walinihakikishia kwamba asitokee mtu yoyote akakwambia kwamba toa kiasi fulani ili tukuletee bajaji yako, na kweli nimeshuhudia mpaka hapa ninapokabidhiwa leo sijatumia hata shilingi moja zaidi ya ile niliyotumia kwa ajili ya ubashiri na kupata tiketi ya kushiriki kwenye huu mchezo (droo).
"Na bahati nzuri (TVS king) imeingia wakati huu ambao mvua zinanyesha nadhani itakuwa "option" nzuri zaidi ya kuweza kujipatia kipato zaidi.
"Yawezekana mwanzoni ukaona kama unapoteza, unaweza ukashiriki lakini naamini siku ikifika unaweza ukasahau na kuamini ukweli kwamba kumbe michezo hii ina faida yake" alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment