December 17, 2017




Wawakilishi pekee wa Tanzania waliokuwa wamebaki katika michuano ya Chalenji, wamefungwa katika fainali kwa mikwaju 3-2 ya penalti na wenyeji Kenya ambao wamekuwa mabingwa.

Zanzibar, ilionyesha soka safi zaidi ya wenyeji Kenya kwenye Uwanja wa Manchakos na kufanikiwa kutoka nyuma mara mbili na kusawazisha mabao.

Kenya walianza kufunga Zanzibar wakasawazisha, Makame Khamis akifunga mabao yote mawili upande wa Zanzibar Heroes na mwisho wa dakika 90, ikawa mabao 2-2.

Lakini upigianaji wa mikwaju ya penalti, Adeyum Seif aliyeingia dakika za nyongeza alikosa na mwisho Mohamed Issa 'Banka’ naye alikosa penalti zao zikipanguliwa na Wakenya wakafanikiwa kuibuka na ushindi huo wa mabao 3-2.


Zanzibar walionyesha soka la kitabuni tokea mwanzo na wachezaji wake walijituma kama ilivyokuwa tokea mwanzo katika michuano hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic