January 21, 2018Kiungo James McCarthy wa Everton sasa atakaa nje na kuukosa msimu wote huh baada ya kuvunjika mifupa miwili ya mguu wake.

McCarthy amevunjika wakati timu yake ikiivaa Wes Brom na Solomon Rondon ndiye aliyemvunja mguu.

Rondon alikuwa akijaribu kupiga mpira lakini akaukuta mguu wa McCarthy.

Baada ya kugundua alikuwa amevunjika mguu McCarthy, Rondon aliangua kilio muda wote hali iliyofanya wachezaji wenzake na hata kocha na madaktari kuanza kumbembeleza. 

Mechi hiyo ambayo Everton ilikuwa nyumbani iliisha kwa sare ya bao 1-1, wenyeji wakisawazisha.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV