January 21, 2018


Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali alionekana kutoridhishwa na kiwango cha vijana wake na kusema atalifanyia kazi.

Wiki tote hii amekuwa busy katika zoezi la kuhakikisha anapandisha kiwango chao kikiwemo cha kipa namba moja Youthe Rostand.

Baada ya kazi yake hiyo, Pondamali ataangalia kazi yake aliyoifanya imekuwa na matunda gani katika mechi ya leo Yanga ikiivaa Ruvu Shooting.

“Pale nitaangalia kama kuna mabadiliko na kama kuna kitu nimeona si sawa, basi tukirudi mazoezini tunaendelea kukifanyia kazi,” alisema.



Pondamali amekuwa akionekana hataki utaki kutokana na kuwapa mazoezi mbalimbali makipa wake akiwemo Beno Kakolanya ambaye amerejea kazini baada ya ule mgomo wake akitaka kulipwa fedha zake.

Kocha huyo wa makipa wa Yanga pia amewahi kuwa kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic