Ikiwa ndiyo siku ya kwanza anaichezea Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, mshambuliaji Obrey Chirwa amekosa penalti ya mwisho na kuing’oa Yanga katika michuano ya Mapinduzi.
URA ya Uganda imeitoa Yanga kwa mikwaju 5-4 na kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mapunduzi.
Mwaka 2016, URA iliing’oa tena Yanga katika hatua hiyo kwa mikwaju ya penalti.
Chirwa alikuwa amegoma kujiunga na Yanga akitaka alipwe fedha zake za usajili. Lakini leo ameungana na kikosi hicho akitokea Dar es Salaam.
Ikiwa ndiyo siku ya kwanza amejiunga na Yanga, Chirwa alitokea benchi kuchukua nafasi ya Pius Buswita na dakika 90 zikaisha kwa sare ya bila mabao, ikaingia mikwaju ya penalti.
Chirwa ndiye alikuwa wa mwisho upande wa Yanga baada ya Papy Tshishimbi, Hassan Kessy, Raphael Daud na Gadiel Michael kupata.
Ni dhahiri,kugoma kwa Chirwa na kuamua kulima matikiti huko kwao,kumeshusha uwezo wake kimpira.Ilihitaji kuwa na kocha mbumbumbu tu kumwamini Chirwa kucheza katika nafasi muhimu na kupewa nafasi ya kupiga peneti katika SAA muhimu kama ile.kutoka kwenye matikiti had I hadhi ya kuaminiwa kupiga peneti sio mbinu ya kocha yoyote finiani.Niliiangalia timu ikimenyana na URA kwa jasho kwelikweli na bidii,hakika wachezaji walijitabifi,lkn Chirwa amezimwaga jitihada za wenzake jalalani, tangu kuanza kwa mashindank hao.
ReplyDeleteNavutwa kuamini kuwa Shadrack na wenzake Wa bench LA ufundi sio waliomtaka Chirwa wakati huu muhimu.bilashaka no pfesha ya mashabiki na dili za wapiga pesa wanao myumia vibayz Chirwa.Huo ndio mpira Wa bongo.wachezaji hupangwa na masgabiki wapiga dili.
Shadravk amesafiri na timu ya chipukizi vixuri sana tangu mwanxo Wa mashindano hayo,hats ufundi Wa amtoe nani aingizwe nani akaongezee kikosi nguvu Shadrack aliweza kuijenga timu take vena,lkn ujio Wa Chirwa umeumiza miogo ya wengi.
Poleni wanatanga.tunayotimu na vijana chiphkizi wazuri ambao wanasimamiwa vizuri sana na Ajibu pale mbele,vijana hao wapya wapewe nafasi na uxoefu watafanya vena.Acheni kufikitia majina ya Wa wachezaji.Kwa vyovyote huwezi kumlrta mdeni wako akuokolee mtoto anaye kanyagwa na ng"ombe.Hugo atasaidia kuua mwanao tu.ndivyo ulivyofanyika kwa Chirwa.Hakukosa peneti ile kwa bahati mbaya,Bali alipanga kumwaibisha mdeni wake.Kesho tujifunze.