January 19, 2018


Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba, imetangaza kuunda Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa Wachezaji ili kujenga nidhamu ndani ya timu yao.

Katika Kamati ya Nidhamu kwa Wachezaji, mwenyekiti wake atakuwa Suleiman Kova akisaidiwa na Robert Selasela, Asha Muhaji, Steven Ally na Suleiman Ally.

Pamoja na kamati hiyo, Kamati ya Maadili kwa viongozi itaongozwa na mwenyekiti, Aziz Kifile, wajumbe ni Alhaji Hassan Mgimu, Malota Soma, David Mihambo na Egbert Muhaga.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kamati hizo zimeundwa ili kuifanya klabu hiyo kuendeshwa kisasa zaidi na kuwepo kwa nidhamu kwa jumla.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic