January 28, 2018



Uwezo aliouonyesha Shomari kapombe baada ya kuingia katika mechi iliyopita, umempa uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza chini ya Mfaransa, Pierre Lechantre.

Kapombe ambaye amekuwa majeruhi kwa zaidi ya nusu msimu wote, alirejea na kusababisha bao wakati Simba ikiitwanga Kagera Sugar kwa mabao 2-0 kwao Kaitaba, Bukoba.

Beki huyo wa kulia, tokea amejiunga Simba kwa mara nyingine amekuwa akihangaishwa na majeraha ya mguu.

Lakini Lechantre alimshuhudia kupitia runinga wakati anaingia kuchukua nafasi ya Nicholas Gyan raia wa Ghana na hakuna shaka leo ataanza na Kapombe katika nafasi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic