Mashabiki wa Yanga wameonekana kushindwa kujizuia baada ya kumvurumishia maneno makali mshambuliaji wao, Obrey Chirwa.
Chirwa amekutana na kadhia hiyo wakati Yanga ikiwasili kutoka Zanzibar ilipokuwa ikishiriki michuano ya Mapinduzi kabla ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali.
Yanga imetolewa baada ya kufungwa penalti 5-4 na URA ya Uganda na Chirwa ndiye aliyekosa mkwaju wa mwisho.
Mashabiki hao walionekana kumlaumu Chirwa kukosa uchungu na Yanga huku wakimueleza kwamba ametanguliza fedha mbele.
Mshambuliaji huyo raia wa Zambia amejiunga na Yanga siku ya ambayo ilitolewa na URA akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa amekaa siku moja tu baada ya kuwasili akitokea kwao Zambia.
Chirwa aliamua kubaki Zambia akishinikizwa kulipwa fedha zake za usajili.
0 COMMENTS:
Post a Comment