Kikosi cha Simba kinatarajia kuanza mazoezi yake leo jioni kujiandaa na mechi ijayo ya Ligi kuu Bara dhidi ya Singida United.
Simba itaivaa Singida United katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Alhamisi ijayo.
Simba imerejea jijini Dar es Salaam baada ya kung’olewa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea mjini Zanzibar.
KIkosi hicho sasa kimebakiza Ligi Kuu Bara pekee ambako watapambana kupata ubingwa baada ya kuwa wamevuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho.
Simba watafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam ikiwa ndiyo mazoezi ya kwanza tokea warejee jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment