January 21, 2018






MPIRA UMEKWISHAAAA

DAKIKA 5 ZA NYONGEZA

Dk 90, Buswita yuko chini pale na kitengo cha ufundi cha Yanga wako pale wakimpatia matibabu, anatolewa nje kwa machela
DK 88, krosi safi ya Martin, Mahadhi yeye na nyavu, anapaishaa puuuuuu


SUB Dk 86 Daud anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Pato Ngonyani, Yanga wakiimarisha ulinzi
SUB Dk 81 Abdulrahman Mussa anakwenda nje Hamisi Mcha anachukua nafasi yake
Dk 80, Yanga wanacheza kindava nje kidogo ya nje ya lango lao. Inachongwa faulo, shuti kali linapigwa, goal kick
Dk 78, Bofu anageuka vizuri, anapiga krosi safi, al manusura iingia nyavuni 
Dk 77 Mahadhi anaingia vizuri kabisa, Shooting wanaokoa na kuwa kona, inachongwa lakini haina madhara


Dk 73, Ruvu wanapata kona hapa, inachongwa vizuri, Kanduru anaachia mkwaju, goal kick
Dk 71, Dante yuko chini baada ya kusukumwa na Kanduru
SUB Dk 70 Buswita analambwa kadi ya njano baada ya kuchomekea mguu Zahiri
SUB Dk 68 Tambwe anakwenda benchi upande wa Yanga, nafasi yake inachukuliwa na Juma Mahadhi
KADI D 67, Mwamuzi anatoa kadi kwa Damas Mwakwaya baada ya kumsukuma Ajibu na mashabiki Yanga kulalamika
KADI Dk 66, Ajibu analambwa kadi ya njano kwa kumsukuma beki wa Shooting
Dk 64, shambulizi kali la Ruvu, pasi nzuri Kanduru yeye na kipa, anamlamba chenga na mpira unaokolewaaa hapa
Dk 63 Yanga wanarudi tena, Buswita anaachia shuti kali kabisa, kipa anadaka vizuri


Dk 62 Kessy anaingia, anamimina krosi safi kabisa, Shooting wanaokoa, inachongwa kona vizuri wanaokoa tena
Dk 59, krosi nzuri ya Abdurahman Mussa lakini wenzake wanachelewa na mpira unakuwa goal kick
KADI Dk 56, Dante analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe dhidi ya Kanduru
Dk 53, Shooting wanaingia vizuri kabisa, lakini Amani anapaisha juuuu
Dk 50 kipindi cha pili kinaonekana kuwa na presha zaidi, ndani ya dakika 5, mashambulizi mawili kila upande
DK 47, nafasi nzuri kwa JKT lakini hawako makini
Dk 45 Yanga wanaanza kwa kasi na kuingia kwenye lango la Ruvu



MAPUMZIKO

-GOOOOOOOOOOO Buswita anafunga bao saafi kwa kichwa akiunganisha krosi ya Ajibu
-Amani anakosa bao peke yake na nyavu baada ya pasi nzuri ya Kanduru

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45 Mussa anaachia mkwaju mwingine mkali tena hapa, Youthe anadaka
Dk 43, Ajibu anaingiza mkwaju vizuri kabisa lakini Zahiri anaokoa na kuwa kona. Inachongwa na Ajibu lakini fauloo
Dk 40 hadi sasa hakuna shambulizi kali kutoka upande wowote na mchezo umepoooza
Dk 39, Kitala yuko chini akitibiwa baada ya kugongana na Kessy
Dk 36 Abdulrahman anaanguka ndani ya eneo la 18, mwamuzi anamuambia "acha zako", kazi inaendelea
Dk 34, Ajibu nje ya 18, anajaribu mkwaju hapa lakini unaonekana hauna macho
Dk 31, Rostand anaruka juu na kuiwahi krosi nzuri ya Amani katikati ya goli lake
Dk 28 Ajibu anachonga kona fupi, Mwinyi anaunganisha krosi safi, Tambwe anaipiga lakini kipa anafanya kazi ya ziada kuukoa
Dk 27 Krosi safi ya Kessy, Amani anaruka juu na kuugusa na kuwa kona ya kwanza ya Yanga
Dk 27, mpira wa kwanza, Martin anaachia mkwaju hapa kipa anadaka
SUB Dk 26, Nkomola anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 25 Abdulrahman Mussa, anaachia mkwaju mkali ndani ya 18 lakini anapaisha juuu
Dk 24, Damas Makwaya anamlamba ngwara Tambwe hapa, mwamuzi anatoa onyo la mdomo
Dk 22, Nkomola anaonekana anachechemea na inawezekana akabadilishwa
Dk 21, Tshishimbi anaachia shuti kali nje ya 18, goal kick
Dk 20 sasa, tahadhari ni kubwa sana kwa kila upande katika ulinzi na mapambano makali yako katikati ya uwanja
Dk 16, Raphael anaingia vizuri na kuachia shuti kali hapa, goal kick


Dk 14, Bofu anamuweka chini Nkomola, yuko anatibiwa nje
DK 10 sasa, mpira zaidi bado unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi kamali
Dk 7, Kanduru anajaribu kuingia upande wa kushoto lakini krosi yake dhaifu kabisa
Dk 6, Ajibu anaingia vizuri kabisa lakini mpira wake unatoka nje na kuwa goal kick
Dk 3, Ruvu wanaata kona ya kwanza baada ya kushambulia mfululizo, inachongwa lakini haina msaada wowote
Dk 1, JKT wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Yanga lakini hakuna madhara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic