January 30, 2018




Simba ina mwendo wa kimondo kutokana na kufanikiwa kushinda mfululizo.

Katika mechi tatu, imekusanya pointi 12 na mabao 12 ukiwa ni wastani wa juu kabisa wa Ligi Kuu Bara. Lakini Masau Bwire anasema, wakati wa ukombozi kwao umfika.

Bwire anasema, umefika wakati wa kuisimamisha Simba ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja na wajue ndiyo ule wakati wa kulipa kisasi.

Katika mzungumzo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Simba ilitwanga Shooting kwa mabao 7-0. Lakini Bwire anawaambia Simba, Ruvu Shooting hii si ile. Hivyo mechi ijayo, watarajie kipigo.

“Tuna morali ya kutosha kwa sasa, hasa baada ya kufanya vizuri kwenye mechi yetu iliyopita dhidi ya Mbao FC, na sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye mchezo ujao dhidi ya Simba ambao tumewapania kuwaonyesha kwamba kwa sasa ni bora tofauti na mwanzo ambapo walitufunga mabao 7-0.


“Tunataka kulipiza kisasi kwa wakati huu na hilo linawezekana kwa sababu kocha Abdulmutik Haji anaendelea kuwanoa vijana ili waweze kufanya makubwa kwenye mchezo huo, hao Simba wajipange kwelikweli kwa sababu tunataka kufanya vizuri kwa sasa ili kubakia kwenye ligi kwa msimu ujao,” alisema Bwire.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic