January 21, 2018PICHA YA MAKTABA, SIMBA WAKIJIFUA UWANJA WA UHURU


Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba watafanya mazoezi yao asubuhi ya leo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Simba iko katika maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambao utachezwa kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Huenda yanaweza kuwa mazoezi ya mwisho ya wachezaji hao na jioni wapata mapumziko.

Simba imerejea Bukoba kuivaa Kagera ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabaoo 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Kocha Masoud Djuma amesema kikosi chake kitapambana kuhakikisha kinapata pointi tatu muhimu kwa kuwa wanajua umuhimu wa kufanya hivyo na kujiweka vizuri zaidi kileleni.


1 COMMENTS:

  1. Saleh jembe tusaidie kumwambia Mo Ibrahim apige tizi yaani kaisha hadi anaboa. Siku hizi natamani hata asipate no simba yani kapoa hana kasi,anatoa pasi za kurudi nyuma kama mkongwe anayeogopa kuumizwa.Asipojituma naona amekaribia kuondoka msimbazi.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV