Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, atakuwa Mgeni Rasmi wakati Simba ikiivaa Gendamarie ya Djibouti katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.
Mwinyi amekuwa mmoja wa mashabiki wakubwa wa mchezo wa soka na watu wanaoamini mazoezi kwa ajili ya afya.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amethibitisha, kuwa Mwinyi atakuwa mgeni rasmi.
Simba itakuwa na kibarua cha kuivaa Gendamarie ambayo inatarajia kutua nchini Jumamosi ikiwa ni siku moja kabla ya mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment