Kiungo Jonas Mkude alifanikiwa kupata usafiri na kuungana na wenzake mjini Shinyanga akipitia Mwanza.
Mkude aliachwa na ndege wakati Simba ikiondoka kwenda Shinyanga kuivaa Mwadui FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Baadhi ya wadau wamelaani kitendo hicho cha Mkude kuchelewa ikionyesha kama si mtu makini.
Hiyo inatokana na Mkude kuingia kwenye tabia hiyo baada ya hivi karibuni kuchelewa mazoezini.
Simba inaivaa Mwadui FC mjini Mwadui, nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga.
Tayari Simba wako kileleni mwa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 41 wakifuatiwa kwa karibu na watani wao yanga wenye pointi 37 baada ya kushinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji, jana.
0 COMMENTS:
Post a Comment