Mabao mawili ya Yanga yaliyofungwa wakati timu hiyo ikishinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji ya Songea katika mechi ya Ligi Kuu Bara, jana, yamezua mjadala.
Mjadala wa wadau wa soka nchini katika mitandao mbalimbali ni kuhusiana na mabao ya Emmanuel Martin na Papy Tshishimbi.
Wachezaji hao wawili, kila mmoja alifunga bao kwa shuti kali na kuamsha hisia za mashabiki wengine wakiamini lile la Tshishimbi ni bora zaidi na wengine wanaona lile la Martin lilikuwa bora zaidi.
Wadau hao kupitia mitandao ya Facebook na Whatsapp walikuwa wakichangia na kila mmoja aliamini tofauti hadi kufikia wakati mwingine kusigana.
Katika mchezo huo, Tshishimbia raia wa DR Congo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
all goal is best
ReplyDelete