February 15, 2018




Kamati ya mashindano ya TFF iliyokutana Februari 13, 2018 pamoja na mambo mengine ilipitia taarifa za mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam kati ya Green Warriors na Singida United.

Deus Kaseke wa Singida United na Shaban Dihile wa Green Warriors wamefungiwa mechi tatu (3) na faini ya shilingi laki tano(500,000) kila mmoja kwa kosa la kutoingia uwanjani na timu zao na hawakuwepo wakati timu hizo zikipeana mikono kwenye mchezo uliozikutanisha timu hizo Januari 31,2018 mchezo namba 73 uliochezwa Azam Complex Chamazi.

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya ASFC(1) ambayo inaelekeza kutumika kanuni ya ligi husika na hivyo kanuni iliyotumika ni 37(7d).
Mchezaji wa Singida United Kambale Salita amepelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga mchezaji wa timu pinzani kwenye mchezo huo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic