February 4, 2018




Kocha maarufu nchini, Abdallah King Kibadeni amesema ana imani kwa asilimia kubwa Simba watakuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

Hata hivyo, amesema itawezekana tu kama kweli wataendelea na mwendo walionao.

"Lazima waendelee kama sasa, washinde mfululizo na ikitokea wamepoteza au kupata sare wasipotee katika njia yao sahihi.

"Kwa sasa Simba ina morali kubwa, hofu yangu wao wenyewe wasitibuane na hasa viongozi. Ikitokea wakatibuana, basi ujue wao watavurugana wenyewe," alisema.

"Katika hivi timu kubwa suala la ugomvi ni wakati wowote na likitokea linavunja umoja, hivyo ni lazima walipe kipaumbele kama jambo muhimu na kuepusha lisitokee."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic