February 4, 2018





Wakati muda ukiwa unakaribia kabla ya Simba kuivaa Ruvu Shooting, msemaji wa timu hiyo ya jeshi, Masau Bwire bado ana uhakika, mnyama "anakufa".

Bwire amesema wamejiandaa kuliko siku zote watu wanavyowajua na nafasi ya ushindi wanaamini ipo.

"Acha watudharau kwa kuwa tuko mkiani, lakini sisi mechi nyingine inakuwa ni siku mpya. Hivyo leo Simba hawatatoka," alisema.

Pamoja na mwendo kasi wa Simba ambayo ndani ya mechi nne imeshinda zote na kufunga mabao 12, yeye bado anaamini nafasi ya ushindi kwao ni kubwa sana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic