MKWASA ALALAMIKIA KUBANWA KWA RATIBA YA LIGI NA FA, UONGOZI KUTUMA MALALAMIKO TFF
Na George Mganga
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amelalamikia namna ratiba ya Ligi ilivyowabana kutokana na uchovu wa wachezaji wake.
Mkwasa amesema ratiba ya michezo inayofuata katika Ligi na Kombe la Shirikisho hapa nchini imewabana, kiasi ambacho wanashindwa kupata mapumziko.
Yanga imetoka kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St, Louis FC ya Sychelles, na sasa inatakiwa kusafiri kusafiri mkoani Songea kwa ajili ya mechi ya FA dhidi ya Majimaji FC February 25
Ratiba vilevile inaonesha baada ya mechi hiyo, Februay 28, Yanga itaelekea Mtwara kucheza na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa klabu umepanga kufikisha malalamiko yao TFF ili wapate urahisi katika ratiba hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment