Pamoja na uongozi wa Simba kusema kwamba tayari kiungo wake Haruna Niyonzima amesafiri kwenda India kwa ajili ya matibabu, taarifa za uhakika zinasema yuko jijini Dar es Salaam.
Awali, Msemaji wa Simba, Haji Manara alisema Niyonzima tayari yuko nchini India.
“Kweli wamesema yuko India, lakini yuko hapa nchini anaendelea na mambo yake. Bado hajapelekwa India kama inavyoelezwa,” alisema.
Haruna amekuwa akisumbuliwa na goti kwa muda mrefu na alitakiwa kutibiwa nchini India.
Simba mpelekeni Niyonzima akatibiwe. Hatuwezi kushindwa kumpatia pesa ya matumizi yake kule. Muhimu aende kupatiwa matibabu haraka iwezekanavyo.
ReplyDelete