YANGA KUPANDA NDEGE KUELEKEA SONGEA KESHO, NI VITA DHIDI YA MAJIMAJI, NI KOMBE LA FA
George Mganga
Kikosi cha Yanga kinatarajia kukwea pipa kesho kueleka mkoani Songea kwa ajilia ya mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Yanga itacheza na Majimaji FC katika Uwanja wa Majimaji mjini humo siku ya Jumapili, terehe 25 March 2018.
Yanga inaenda kucheza na Majimaji ikiwa imetoka kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo ilifanikiwa kusonga mbele kwa kuiondoa St. Luois FC ya Ushelisheli.
Mbali na mechi hiyo, mechi zingine zitakazopigwa siku hiyo ni Buseresere watakuwa uwanja wa Nyamagana Mwanza saa 8 mchana kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Vilevile Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania saa 1 usiku Azam Complex Chamazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment