Aliyewahi kuwa kipa namba moja wa timu ya soka ya St George ya Ethiopia, Ivo Mapunda, anaamini Yanga watafanya vizuri katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Welayta Dicha ya nchini humo endapo wataonyesha nidhamu ya mchezo.
Juzi, Jumatano, Yanga ilipangwa kucheza dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia katika droo ya Hatua ya Mtoano ambayo ilifanyika jijini Cairo nchini Misri.
Mapunda ambaye alitamba St George aliyojiunga nayo mwaka 2008 akitokea Yanga, alisema timu hiyo ni nzuri na ina uwezo mkubwa wa kucheza soka, hivyo endapo Yanga wataonyesha nidhamu ya mchezo anaamini watafanya vizuri.
“Yanga wasibweteke na kuona kuwa wamepangiwa timu kibonde, wanatakiwa kujipanga na kuiheshimu timu hiyo.
“Wanapaswa kujua aina ya soka la Ethiopia ambalo huwa ni la kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa, kama wasipojipanga, balaa linaweza kuwakuta kama imeweza kuitupa nje ya michuano hiyo Zamalek ya Misri, siyo timu ya kubeza,” alisema Mapunda.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Sasa hii habari na mlichokiandika headline mbona haviendani?pumbavu kabisa
ReplyDeleteSasa hii habari na mlichokiandika headline mbona haviendani?pumbavu kabisa
ReplyDeleteni kweli asee
ReplyDelete