AL MASRY KUTUA NCHINI SIKU HII KUJA KUIKABILI SIMBA KOMBE LA SHIRIKISHO, VIINGILIO VYATAJWA
Na George Mganga
Kikosi cha Al Masry kinatarajia kuwasili nchini wiki hii kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba SC, mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema Al Masry watatua nchini, jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba, na watafanya mazoezi kufanya mazoezi Jumatatu jioni katika Uwanja wa Taifa.
Kuelekea mchezo huo, Haji Manara amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu kwa njia ya Selcom ambapo viingilio vitakuwa ni 5000 kwa Mzunguko na Orange, 15,000 VIP B na 20,000 VIP A.
Mchezo huo utachezwa Machi 7 2018 kuanzia saa 12 jioni ili kuwapa fursa wfanyakazi kwenda kuitazama mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment