March 6, 2018


Na George Mganga

Baada ya kikosi cha Yanga kitakachocheza dhidi ya Township Rollers FC kuwekwa hadharani, mashabiki wa timu hiyo wamekuja juu wakililalamikia benchi la ufundi.

Mashabiki hao wamecharuka wakihoji imekuwaje kiungo Thaban Kamusoko aachwe ilihali awali ilitangazwa kuwa atakuwepo katika mchezo wa leo.

Kupitia kurasa za timu hiyo ambazo zipo Facebook, Instagram na Twitter, maoni mengi yaliyowekwa na wapenzi wa timu hiyo yamelalamikia viongozi huku wengi wakisema ubabaishaji umefanyika.

Taarifa za awali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, zilisema kuwa Kamusoko ni moja ya wachezaji walio fiti asilimia 100 kucheza leo, japo mambo yamekwenda mrama.

Hatua hiyo imechukua taswira mpya kwa mashabiki huku baadhi wakitoa maoni yao kwa kuandika maneno makali na baadhi wakisema viongozi wao wamekuwa waongo.

Yanga itakuwa Dimbani jioni ya leo kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Bostwana, mechi itaanza saa 10 kamili jioni.

1 COMMENTS:

  1. Kazi ya uandishi sio kuwa reporter tu bali pia kuwa mchambuzi. Usiseme mashabiki bali tumia neno baadhi ya mashabiki kwasababu wapo wanaoelewa. Mchezaji hata kama yuko fit lazima ujue hakuwa uwanjani kwa zaidi ya miezi mitatu. Maandalizi ya mechi hayafanyiki siku moja au wiki moja bali ni mwendelezo wa mafunzo na makosa mbalimbali yaliyokuwa yakirekebishwa. Yes, yuko fit 100% lakini bado sio sehemu ya mfumo aliouandaa mwalimu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic