March 6, 2018


Na George Mganga

Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amemuomba Katibu Mkuu wa klabu hiyo kuacha kuudanganya umma.

Kauli ya mzee Akilimali imekuja mara baada ya kikosi cha leo kitakachocheza dhidi ya Township Rollers FC kuwekwa wazi huku baadhi ya wachezaji waliotajwa kuwepo wakikosekana.

Katika mkutano alioitisha jana na waandishi wa habari, Katibu Charles Mkwasa, alisema wachezaji Thaban Kamusoko, Yohana Nkomola pamoja na Ramadhan Shaibu 'Ninja' watakuwa fiti asilimia 100 kucheza leo.

Akilimali amemuomba Mkwasa kuwa mkweli haswa linapotokea suala la mechi za kimataifa, kwani huhitaji kikosi chenye wigo mpana na si kuwadanganya watu kuwa fulani atakuwepo kisha baadaye akosekane.

Na kuelekea mchezo wa leo, Akilimali amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa hamasa timu yao, ili iweze kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika.


1 COMMENTS:

  1. Muhimu kuamini kwamba Yanga ilisajili wachezaji na si watazamaji wa mpira na kwamba washabiki na waoenzi wawe na imani na kikosi chao......kuanza malumbano sasa licha ya kukatisha tamaa wachezji wengine ni kukosa dira ya lawama........zaidi ya yote Mkwasa kama Katibu Mkuu anapokea taarifa ya daktari na kuwajuza wanayanga, mengine yooote ni ya KOCHA yaani hapo ni sawa na kusema Mkwasa kwa alichosema alazimishe pia wachezaji hao wapangwe kikosi cha leo ....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic