March 14, 2018


Baada ya kutupiwa virago kwenye mashindano ya UEFA Champions League usiku wa jana dhidi ya Sevilla kutoka Spain, Kocha Jose Mourinho, asema ni kitu cha kawaida.

Mourinho ameshindwa kuungana na Liverpool pamoja na Manchester City kuelelea safari ya 8 bora baada ya kipigo cha jana kutoka Sevilla.

Kufuatiwa kuondolewa, Mourinho ameeleza hakuna kitu kipya kuondolewa kwa United katika raundi ya 16 kwani ni jambo la kawaida kwenye mpira.

"Sidhani kama kiwango chetu hakikuwa kizuri, tumepoteza kwenye hatua hii ya 16 bora kwa mara ya nne.

Aliongezea: "Sijutii, nilionesha kilicho bora kwangu na wachezaji walionesha ubora wao, tulijitahidi na tumepoteza, huo ndiyo mpira." alisema Mourinho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic