NENO KUTOKA AZAM FC KWA YANGA NA SIMBA KUELEKEA MECHI ZAO ZA KIMATAIFA
Na George Mganga
Baada ya Yanga kukwea pipa na kufika salama nchini Botswana ambapo watakuwa wana kibarua kizito dhidi ya Township Rollers kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba nao wanatarajia kuondoka leo.
Simba wataondoka kuelekea Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Al Masry, mchezo ukiwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Kufuatia uwakilishi wa timu hizo pekee mbili kwenye mashindano ya kimataifa kutoka hapa Tanzania, Klabu ya Azam imetoa baraka zake kwa timu hizo mbili.
Akizungumza na Saleh Jembe, Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga, amezitakia kheri timu zote mbili ambazo zinaiwakilisha nchi.
Maganga amesema Simba na Yanga wanapaswa kupambana katika michezo hiyo kwa maana itakuwa migumu kwani hata wao waliwahi kushiriki.
"Sisi tunawatakia kila la kheri, tunajua wanaiwakilisha Tanzania na hatuna budi kuwatakia mema, kifupi wakapambane washinde" alisema.
Yanga na Simba watacheza dhidi ya wapinzani wao Jumamosi hii ya Machi 17 2018.








0 COMMENTS:
Post a Comment