BAADA YA KUSHANGILIA MABAO YA MESSI DHIDI YA CHELSEA, FERDINAND ASEMA MESSI NI ZAIDI YA RONALDO, HAYA NDIYO AMEYASEMA
Na George Mganga
Beki aliyewahi kuichezea Manchester United, Rio Ferdinand, juzi alionesha kushindwa kuzuia hisia zake kwa nyota wa FC. Barcelona, Lionel Messi.
Tukio lilitokea katika mchezo wa marudiano kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya wakati wa mechi ya vinara hao wa Ligi ya Spain dhidi ya Chelsea, mechi ambayo Barcelona ilishinda kwa mabao 3-0.
Ferdinand alionekana akishangilia mabao mawili aliyofunga mchezaji huyo pamoja na namna kiwango chake kilivyokuwa.
Pamoja na hayo, Ferdinand amesema Messi na Ronaldo wote ni wachezaji wazuri lakini utofauti wao ni kwamba, Ronaldo anapokuwa langoni kwa mpinzani wake akili yake hufikiria kufunga tu.
Aidha Ferdinand amesema, Messi ni mchezaji ambaye anaweza akatoka na mpira katikati ya Uwanja akicheza kama kiungo, na akipandisha mashambulizi huku akipasiana na wenzake, mchezaji ambaye analeta ladha ya mchezo uwanjani.
Vilevile alieleza kuwa Messi ni mchezaji ambaye hawezi akakuruhusu kuusogelea mpira na kumgusa, huku akikumbushia mara ya mwishi walipokutana na Barcelona wakati akiwa Manchester United kuwa hakumbuki kama aligusa mguu wake.
Ferdinand anaamini Messi ni bora kuliko Ronaldo kutokana na mchezaji huyo kuwa na vitu vingi Uwanjani, lakini akisema wote ni wazuri.








0 COMMENTS:
Post a Comment