BOCCO ASEMA SIMBA INA HISTORIA KUBWA KATIKA SOKA LA AFRIKA, WAKO TAYARI KWA MAPAMBANO, OMBI LAKE KWA MASHABIKI HILI HAPA
Na George Mganga
Mshambuliaji wa Simba anayefanya vizuri ndani ya timu hivi sasa, John Bocco, amesema kuwa Simba ina historia nzuri katika soka la kimataifa.
Bocco amesema hayo kutokana na timu hiyo kuwahi kufika katika fainali ya mashindano ya CAF mwaka 1993 iliyopigwa Shamba la Bibi ama Uwanja wa Uhuru dhidi ya Stella Abdijan.
Aidha mshambuliaji huyo amesema hawakufanya vema katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United ya Shinyanga, hivyo amesema watatumia makosa ya mechi hiyo kesho dhidi ya Al Masry SC.
Bocco ameeleza ni wakati mwafaka wa kufanya vema mechi ya nyumbani ili wakienda ugenini wasije wakapata ugumu wa kusonga mbele.
Vilevile Bocco hakuishia hapo bali amewaomba mashabiki kujitkkeza kwa wingi kesho uwanjani ili waweze kuipa sapoti timu yao.
Local League huwezi kufananisha na mechi ya Kimataifa namaanisha makosa ya Stand United yasitumike kwa Al Masry....otherwise kila la heri YANGA NA SIMBA
ReplyDelete