March 6, 2018


Na George Mganga

Kocha Mkuu wa Simba SC, Pierre Lechantre, amesema kuwa analijua soka la Misri hivyo amewaomba mashabiki ni vema wakajitokeza mashabiki kwa wingi kesho kuipa hamasa timu.

Lenchantre ameeleza kuwa anawatambua Wamisri wapo vizuri hivyo watapmbana kuhakikisha wanapata matoko.

Aidha, Kocha huyo ameeleza ameshacheza soka la kimataifa, na amefanikiwa kufundisha katika ngazi za juu, hivyo anamesisitiza ujio wa mashabiki kama wachezaji namba 12 uwanjani.

Mbali na hilo, Lechantre amesema pia ni vema wakatumia faida ya uwanja wa nyumbani kushinda ili wakienda kucheza mchezo wa marudiano iwe rahisi kusonga mbele.

Lechantre ameongezea kuwa timu inapotumia uwanja wa nyumbani vizuri, uhakika wa kusonga mbele unakuwepo kutokana na ugumu unaokuwepo mechi za ugenini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic