BREAKING: CARRAGHER ASIMAMISHWA KAZI SKY SPORTS MPAKA MSIMU WA LIGI UTAKAPOMALIZIKA
Uongozi wa Sky Sports TV umetangaza kumsimamisha kazi mchezaji wa zamani wa Liverpool na Mchambuzi wa Soka, Jammie Carragher, mpaka msimu huu wa Ligi Kuu Uingereza utakapomalizika.
Hukumu hiyo imetoka kutokana na Carragher kumtemea binti mwenye miaka 14 ambaye ni shabiki wa Manchester United, mapema wakiwa wanatoka kutazama mchezo Ligi Kuu England kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool.
Awali alisimamishwa kwa muda wa wiki mbili, lakini adhabu hiyo imeongezwa mpaka pale msimu huu wa ligi nchini humo utakapomalizika.
Licha ya adhabu hiyo, Carragher aliomba msamaha kwa binti na familia yake.
Taarifa kwa mujibu wa BBC.








0 COMMENTS:
Post a Comment