TFF YAMPELEKA WAMBURA KAMATI YA MAADILI, SUALA LAKE KUJADILIWA LEO
Kamati ya maadili ya TFF inakutana leo Machi 14, 2018 pamoja na mambo mengine kujadili suala la Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Wambura, aliyefikishwa kwenye kamati kwa makosa matatu.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema kuwa kosa la kwanza analokabiliwa nalo Wambura ni kupokea fedha za TFF. Pili, malipo yasiyo halali na tatu ni kugushi barua na kushusha hadhi ya TFF.









0 COMMENTS:
Post a Comment