Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali amewataka wachezaji wa timu hiyo kuwa makini katika mchezo wa marudiano kwa kutojali fitna watakazofanyiwa na mashabiki wa Al Masry kwa kuwa waliwahi kufungiwa kutokana na vurugu zao.
Simba inatarajia kurudiana na Al Masry wikiendi ijayo baada ya mchezo wa awali waliocheza Uwanja wa Taifa jijini Dar kupata sare ya mabao 2-2.
Dalali alisema kuwa, Simba inatakiwa kucheza mechi hiyo kwa tahadhari kubwa kutoka na ukorofi wa mashabiki wa Al Masry kwa kuwa waliwahi kufungiwa kutokana na vurugu.
“Wachezaji wa Simba wanatakiwa wajiandae kisaikolojia kujua timu ambayo wanakwenda kukutana nayo kuwa iko vipi, mashabiki wa Al Masry ni wasumbufu waliwahi kufungiwa huko nyuma kutokana na kufanya fujo.
“Hivyo wachezaji wanatakiwa kuwa makini watakapokuwa uwanjani na wanatakiwa kuhakikisha hawawasikilizi wao na badala yake wajitume ili kuweza kupata ushindi naamini watafanya vizuri kwani wanayo nafasi ya kusonga mbele,”alisema Dalali.







0 COMMENTS:
Post a Comment