Utakuwa umesikia watu kwamba kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi na kipa Youthe Rostand wa Yanga walishikiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama jijini Gaborone, Botswana.
Wachezaji hao walishikiliwa baada ya Yanga kufika Botswana mara baada ya kutua nchini humo na tatizo liliezwa kuwa ni viza.
Mara baada ya kukamtwa na taarifa kupatikana, zilifuatiliwa na kuripotiwa leo.
Mambo yalikuwa hivi:
Pamoja na Tshishimbi raia wa DR Congo, kipa Youthe Rostand naye ameshikiliwa na Idara ya Uhamiaji ya Botswana ikiwa ni muda mchache baada ya Yanga kuwasili nchini humo.
Yanga iko Botswana kwa ajili ya kuivaa Township Rollers katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mechi ya kwanza ilipigwa jijini Dar es Salaam na Yanga kulala kwa mabao 2-1.
Taarifa za uhakika kutoka Gaborone zimeeleza, wawili hao si raia wa Tanzania na ndiyo chanzo cha kushikiliwa.
“Tumewapokea Yanga na kuwapeleka hotelini lakini Tshishimbi na Rostande wamezuiliwa, bado wanashikiliwa pale uwanja wa ndege kutokana na kutokuwa na visa,” kilieleza chanzo cha uhakika kutoka jijini Gaborone.
“Unajua Watanzania hawaingii na visa hapa Gaborone, lakini Cameroon, Congo na nchi nyingine wanatakiwa kuwa na visa.
“Sasa kukawa na shida kubwa pale, juhudi zimefanyika na imeshindikana, tumewaacha pale. Uongozi wa Rollers ambao ni wenyeji wao wanasema waliwaambia viongozi wa Yanga lakini hawakufuatilia.”
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema tayari wameachiliwa baada ya kila kitu kufanyika.
Mkwasa amesema walifanya taratibu zote lakini kulikuwa na taratibu zao wenyewe.
"Kwanza wameishaachiwa," alisema Mkwasa.







0 COMMENTS:
Post a Comment