March 8, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kesho kinaingia dimbani kucheza na Kagera Sugar katika Uwanja wa Yaifa, Dar es Salaam, mechi ya Ligi Kuu tanzania Bara.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Teni, amesema tayari matayarisho ya mchezo huo dhidi ya Kagera yapo tayari na wamejipanga kupata matokeo.

Teni amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kutokana na imani ya uwepo wao itakuwa chachu ya wao kuipa hamasa timu ili iweze kupata matokeo

"Kwa ujumla matayarisho ya mchezo wa kesho yamekamilika, tni mechi ya nyumbani na tunahitaji kupata matokeo, nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kuisapoti timu, shabiki wa kweli ni yule anayekuja uwanjani kuitazama timu yake" amesema Teni.

Hii itakuwa mechi ya 20 kwa Yanga kwenye ligi msimu huu baada ya kutoka kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrik,a Jumanne ya wiki hii dhidi ya Township Rollers wakipoteza kwa mabao 2-1 nyumbani.

Yanga watakuwa wanapambana na Kagera Sugar kesho, ili kupata matokeo ambayo yataifanya izidi kupunguza uwiano wa pointi na Simba iliyo na 46.

Ushindi wa Yanga kesho utaifanya ifikishe alama 43 na hivyo kupunguza gepu la pointi kutoka 6 za sasa mpaka 3. 

3 COMMENTS:

  1. Mechi ya Azam na Mwadui nimeiangalia. Timu zote zimecheza vizuri. Azam amepata ushindi wa goli 1-0 nalilofunga kijana Yahaya Omari Zayd. Baada ya kufunga goli akafungua bukta yake kiunoni akatoa karatasi iliyokuwa imeandika ujumbe fulani akaenda golini kufungua na kushangilia na wenzie. Mimi nalaani kitendo hicho. Nilitegemea Refarii angempa kadi ya njano. Hivi karatasi ile ilipitaje bila kukaguliwa? jibu aliificha. Je angeweka upupu au unga wa sumu ya kumwagia mchezaji mwenzie au refa? Hapakuwa na sababu ya kufanya vile. Je wachezaji wote wafiche karatasi za namna ile na wanapofunga goli wazitoe? Zayd mchezaji mzuri sana lakini kitendo hiki kina madhara kwenye maadili ya mpira asifanye hivyo.

    ReplyDelete
  2. Kwani hawa yanga wanacheza kesho hawakutaka kupata muda wa kujitaasrisha na mecho yao na Rollers kama ilivo Simba au ndio wameshavunjika moyo kutokana na kungwa?

    ReplyDelete
  3. Yanga anakiporo wakati simba keshacheza mechi moja zaidi ya ligi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic