KIAMA CHA WAMBURA NA TFF KUJULIKANA JUMAMOSI HII
Rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, inatarajiwa kusikilizwa Jumamosi ya wiki hii katika makao makuu ya shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa Wakili Emmanuel Muga anayemtetea Wambura, amesema tayari wameshapokea barua ya wito inayomtaka mteja wake aende na utetezi wa maandishi au kwa njia ya mdomo ili kukamilisha usikilizwaji wa rufaa hiyo.
TFF ilimfungia maisha Wambura kutojihusisha na masuala ya soka nchini kufuatia kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine.
Rufaa itaanza majira ya saa 5 kamili asubuhi kunako Makao Makuu ya Shirikisho hilo yaliyopo mitaa ya Karume, Ilala, Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment