BEKI SIMBA AREJEA KIKOSINI
Ikiwa ni takribani wiki mbili ligi tangu zisimame kupisha mechi za kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, sasa inatarajiwa kuendelea tena siku kadhaa zijazo.
Habari njema kwa mashabiki wa Kagera Sugar ni kurejea kwa beki Juma Nyosso, aliyefungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF baada ya kumpiga shabiki Uwanjani.
Nyosso ambaye aliwahi kuichezea klabu ya Simba, alifungiwa kutocheza jumla ya mechi 5 baada ya kumpiga shabiki aliyemzomea baada ya pambano dhidi ya Simba kumalizika Uwanja wa Kaitaba ikiwa ni Januari 22 2018 katika mchezo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Beki huyo anarejea kikosini huku timu yake ikijiandaa kukabiliana na Ndada FC katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara.
Msimamo wa ligi unaonesha Kagera imekamata nafasi ya 12 ikiwa imejikusanyia alama 21 tangu msimu huu wa ligi uanze.
0 COMMENTS:
Post a Comment