VIINGILIO VYA MCHEZO WA TAIFA STARS DHIDI YA CONGO VYATAJWA, KIKUBWA NI ELFU TANO TU
Viingilio vya mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimetajwa rasmi.
Mchezo huo ambao ni kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, utafanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa, Machi 27 2018.
Viingilio hivyo ni Tshs 5000 kwa VIP A, B na C, huku Mzunguko ikiwa ni Tshs 1000 tu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linawaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa siku hiyo ili kuipa hamasa Taifa Stars.
0 COMMENTS:
Post a Comment